Kumbukizi ya Rais Magufuli alipofanya Maamuzi ya kumpandisha cheo kiongozi wa JWTZ kwa Uwajibikaji.

10 months ago
10

#Magufuli #Tanzania #Magulificationoftanzania #short #shprts #shortvideo #shortsvideo #shorts
Kumbukizi ya Rais Magufuli alipofanya Maamuzi ya kumpandisha cheo kiongozi wa JWTZ kwa Uwajibikaji mzuri.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amempandisha Cheo afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Charles Mbuge kutoka cheo cha Kanali na kuwa Brigedia Jenerali baada ya kupendezwa na namna alivyosimamia na kufanikisha ujenzi wa baadhi ya ofisi za mji wa Serikali Jijini Dodoma pamoja na nyumba za watumishi. Mwezi mmoja uliopita Brigedia Jenerali Charles Mbuge alikabidhiwa kufanya kazi ya ujenzi wa nyumba za Jeshi la Magereza zilizopo eneo la Ukonga Jijini Dar es Salaam ambazo ujenzi wake umekamilika na pia ndiye aliyesimamia ujenzi wa ukuta wa kuzunguka eneo la machimbo ya madini ya Tanzanite, Mirerani Mkoani Manyara.
Apr 13, 2019

Licensed under a Creative Commons AttribushareAlike 4.0 International License. Based on a work at https

Loading comments...