KUSAIDIA WENGINE NI NJIA YA KUPATA ZAIDI | Ejaz Bhalloo Inspiration

2 years ago
4

KUSAIDIA WENGINE NI NJIA YA KUPATA ZAIDI | Ejaz Bhalloo Inspiration

Taasisi ya Ejaz Bhalloo Inspiration ilipata fursa ya kutembelea kituo cha watoto yatima cha Amani foundation pamoja na klabu ya Leo ya Mzizima chini ya taasisi ya Lions Clubs. Katika tukio hilo la kuwafariji watoto wa kituo, tulikabidhi mchele, sembe, maharage na sukari. Pamoja na haya, tuliwapa watoto vitafunwa vikiwemo mandazi, vitumbua, keki, Samosa, biskuti, soda na juisi.

Tuliwapa watoto nguo na kuwalipia bili ya umeme kwa mwezi mmoja. Zaidi ya hayo, watoto walipata fursa ya kusikiliza hotuba za kuvutia zilizotolewa na watu maarufu nchini Tanzania wakiwemo Mr. Shehzada Walli, Inspector Angello, Inspector Jane, Ms. Miriam Mauki, Na Kadhalika. Mkurungenzi wa kituo hicho Bi. Hajat Zubeda ameshukuru kwa msaada huo ambao amesema ni upendo kwa watoto wenye uhitaji.

FOLLOW EJAZ BHALLOO
https://www.instagram.com/ejazbhalloo/

Loading comments...