Bikira Maria Katika Ufalme wa Utashi wa Mungu - Utashi wa Mungu
1 FollowerUtangulizi Makala ya asilia ya andiko hili la Mtumishi wa Mungu Luisa Piccarreta linaonyesha Tarehe 6 Mei 1930. Ni mkusanyo wa Fikara 31 kwa ajili ya siku zote za mwezi Mei. Fikara nyingine zilipatikana kwa peke yake na kwa kipindi tofauti. Fikara hizi zinaleta matukio na mafumbo mengine ya maisha ya Bikira Mtakatifu sana. Kulikuwa na Matoleo matatu ya Kitabu Hiki yakiwa yameratibiwa na kuchapishwa na Padre Benedetto Calvi aliyekuwa ni Padre mwungamishi wa mwisho wa Luisa Piccarreta. - Toleo la Kwanza (1932), lilibeba kichwa hiki: " Bikira Maria Katika Ufalme wa Utashi wa Mungu " - Imprimatur ya Makao Makuu ya kiaskofu ya Montepulciano, tarehe 30 Machi 1932. Sahihi ni ya Askofu Giuseppe Batignani, Askofu wa Montepulciano. - Toleo la Pili (1933), likiwa na kichwa cha " Malkia wa Mbingu Katika Ufalme wa Utashi wa Mungu”. Nihil Obstat quominus riemprimatur" - "Nihil obstat quominus riemprimatur": Taranto, Tarehe 23 Septemba 1933. Sahihi ni ya Mwakilishi wa Askofu Mkuu Giuseppe Blandumura. - Toleo la Tatu (1937) lilibeba kichwa hicho hicho. - "Nihil obstat quominus riemprimatur": Taranto Sikukuu ya Kristo Mfalme 1937, Mons Francesco M. Della Queva. - (Toleo hili la mwisho lilikuwa na Nyongeza kadhaa: "Makuu ya pendo ambayo Utashi wa Mungu umeyatenda ndani ya Malkia wa Mbingu – Nyongeza hiyo ina sura nzuri sana " - kadiri ya sura 20 hivi, zilizochukuliwa kutoka Juzuu za mwishoni mwa Shajara ya Mtumishi wa Mungu, sura ambazo zilichapishwa pia peke yake chini ya kichwa - " Sala za kutwa nzima ya Utashi wa Mungu ", nk.).